Zahera Apata Kigugumizi Mshindi wa Yanga, Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Zahera Apata Kigugumizi Mshindi wa Yanga, Simba-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Yanga ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Gwambina, Mkongomani Mwinyi Zahera ameshikwa na kigugumizi cha kutabiri mshindi kwenye mechi ya dabi kati ya Yanga na Simba.

 

Zahera ameongeza kwamba anashindwa kumtaja atakayeibuka na pointi tatu kwenye mechi hiyo kutokana na timu zote kuwa na asilimia 50 za ushindi kwa sababu ya ugumu na vikosi vizuri walivyo navyo.

 

Yanga leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa watakuwa wenyeji wa Simba kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo inatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa.

 

Zahera ameliambia Championi Ijumaa, kuwa kwake hawezi kumtaja mshindi wa moja kwa moja kwenye mechi hiyo kwa sababu ya timu zote kuwa na asilimia sawa za kupata matokeo.

 

“Mechi hii ya Yanga na Simba ni ngumu na wote wana asilimia 50 kwa 50 za kushinda kwa sababu wote wana timu nzuri. “Kwangu naona yule mwenye plani na nidhamu nzuri uwanjani na atakayefanya vizuri ndiye ambaye atashinda.

Said Ally, Dar es Salaam

The post Zahera Apata Kigugumizi Mshindi wa Yanga, Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz