-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

ALIYEWAHI kuwa Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, jana asubuhi alivamia kambi ya timu yake hiyo ya zamani kwa ajili ya kwenda kusalimia wachezaji wa timu hiyo pamoja na kocha Cedric Kaze muda mfupi kabla ya mechi yao.

 

Yanga ipo jijini Mwanza imeweka kambi katika Hotel ya Capri Point, kwa ajili ya mechi zake tatu za Kanda ya Ziwa, ambapo jana ilimalizia mechi zake kwa kuivaa Gwambina FC ambapo Zahera ni mkurugenzi wa benchi la ufundi la timu hiyo.

 

Zahera aliifundisha Yanga msimu uliopita kabla ya kuondolewa kikosini hapo ambapo alikuwa ni miongoni mwa makocha wenye hamasa kubwa ndani ya kikosi hicho ambacho kilikuwa na ukata wa hali ya juu kulikomsababisha aanzishe mpango wa kutembeza bakuli kwa wadau.

Taarifa ambazo Championi Jumatano, imezipata kutoka kambini hapo ni kwamba, Zahera alifika Capri Point asubuhi ya saa 2:30 ya jana ikiwa ni muda mfupi kabla ya kuvaana na Yanga katika Uwanja wa Gwambina.

 

Aidha Zahera alipata fursa ya kusalimiana na viongozi wa benchi la ufundi pamoja na baadhi ya wachezaji ambao aliwaacha kikosini hapo huku akiwa na furaha kubwa kuwaona wenyeji wake hao wa zamani na kupata nafasi ya kuzungumza mambo mawili matatu.

The post Zahera Amvamia Kaze Kambini Mwanza appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand