-->

Type something and hit enter

On




 HATIMAYE baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takriban miezi minne kufuatia jeraha la kifundo cha mguu, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Balama Mapinduzi anatarajiwa kuanza rasmi mazoezi ya pamoja na wenzake mara baada ya timu hiyo kurejea jijini Dar keshokutwa Jumatano ikitokea Kanda ya Ziwa.

 

Balama alipata jeraha hilo Juni, mwaka huu kwenye mazoezi ya Yanga iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda, ambapo tangu amepata jeraha hilo amekosa michezo 15.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Daktari wa kikosi cha Yanga, Shecky Mngazija alisema vipimo vya hivi karibuni alivyofanyiwa nyota huyo vinaonyesha amepona kwa kiasi kikubwa na muda wowote ataanza mazoezi ya pamoja na timu.

 

“Nyota wetu Balama Mapinduzi anatarajiwa kuanza rasmi mazoezi ya pamoja na wenzake hivi karibuni, hii ni baada ya kiungo huyo kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza jeraha la kifundo cha mguu alilolipata mazoezini mwishoni mwa msimu uliopita.

 

“Vipimo vya hivi karibuni vinaonyesha Balama amepona kwa kiasi kikubwa na tayari alikuwa ameanza mazoezi mepesi peke yake, tunaamini pindi timu itakaporejea jijini Dar es Salaam ataanza mazoezi ya amoja na timu,” alisema Mngazija.

Click to comment
 
Blog Meets Brand