-->

Type something and hit enter

On
 KIKOSI cha Yanga jana Novemba 15 kimeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya African Lyon kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Huu ni mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa Kocha Mkuu, Cedric Kaze baada ya kupokea mikoba ya Zlatko Krmpotic aliyefutwa kazi, Oktoba 3.


Mabao ya ushindi kwa Yanga yamefungwa na Tuisila Kisinda dakika ya 3, Yacouba Sogne dakika ya 7, Michael Sarpong dakika ya 28 kwa mkwaju wa penalti.


Bao la kufutia machozi kwa African Lyon lilifungwa na Mwalami Abdalah kwa mpira wa adhabu dakika ya 30 nje kidogo ya 18 na kuachia shuti lililomshinda mlinda mlango Ramadhan Kabwili.

Click to comment
 
Blog Meets Brand