-->

Type something and hit enter

On
 PISI kali Bongo Muvi, Jacqueline Wolper amesema kuwa anashangaa sana kuona watu wengi wanaisubiria mimba yake kwa hamu wakati mimba za mastaa wengine hajawahi kusikia foleni hiyo ya watu.

 

Akizungumza na MIKITO NUSUNUSU, Wolper amewatoa hofu watu hao kwa kuwaambia, suala la mimba halijifichi kwani kama ipo haiwezi kujificha kwa sababu mimba hainywei bali inakua siku hadi siku hivyo wawe wapole tu mpaka muda utakapofika itaonekana bila kificho au kama ni mtoto, watamuona.

 

“Bado najiuliza maswali mengi sana kwa nini watu wanaisubiria kwa hamu mimba yangu yaani kuna kitu gani cha ziada maana kuna wasanii wengi sana kwa kipindi hiki wamepata ujauzito mbona hawakuwasubiria hivi? Ninachoamini mimi ni kwamba mimba haijifichi hata kidogo, watulie tu,” alisema Wolper ambaye kwa sasa yuko kwenye uhusiano na mfanyabiashara Richie Mitindo na vyanzo mbalimbali vikieleza uhusiano wao umejibu kwa mimba lakini mrembo huyo anaificha.

Click to comment
 
Blog Meets Brand