-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BONDIA Mtanzania, Hassan Mwakinyo ameshinda na kuetetea mkanda wake wa WBF Intercontinental Super Welterweight dhidi ya Jose Carlos Paz raia wa Argentina baada ya kumshinda kwa TKO kunako raundi ya nne tu ya pambano hilo la raundi 12, usiku wa kuamkia leo Novemba 14, 2020.

Pambano hilo lilianza kwa kasi huku Mwakinyo akirusha makonde mazito kwa Muargentina huyo kuanzia raundi ya kwanza tu ya mchezo, lakini ilipofika raundi ya nne, alimtwanga vibaya na kumfanya ashindwe kabisa kuendelea na mchezo huo,  hali iliyompelekea mwamuzi wa mpambano kumaliza mpambano huku Mwakinyo akiendelea kudhihirisha ubabe wake kwenye ngumi katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Pambano hilo lilitanguliwa na mapambano mengine yakiwemo ya wanawake ambapo Mkenya Fatuma Zarika alitwaa ubingwa wa WBF (Kg 57) baada ya kumchapa Mzimbabwe Patience Mastara kwa pointi. Mbali na kutoka sare kwenye pambano lao, lakini vitasa viligongwa kwelikweli kati ya Hussein Itaba dhidi ya Alex Kabangu wa DR Congo.

Baada ya kumazika kwa pambano hilo, Mwakinyo, akituma ujumbe kwa mabondia wanaotamba wakitaka kupigana naye, amesema: “Itakuwa ni mwisho wao kuongea, kwa sababu wao wanacheza na mabondia walevi… Mimi ndiyo Tanzania One.”

TAZAMA VITASA HAPA

The post Vitasa Hatari! Mwakinyo Amfanya Kitu Mbaya Muargentina – Video appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand