-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

 

HABARI njema kwa mashabiki wa Liverpool ni kwamba beki kitasa wa timu hiyo Virgil Van Dijk anatajwa kuanza kufanya mazoezi mepesi yatakayomsaidia kurejea kwenye ubora wake wa zamani.

 

Beki huyo wa kati anasumbuliwa na majeraha ya goti ambapo kwa sasa anapambana ili arejee uwanjani baada ya kuumizwa na nyota wa Everton, Jordan Pickford kwenye Merseyside dabi mwezi uliopita.

 

 

Baada ya kufanyiwa vipimo na upasuaji Van Dijk taarifa zinaeleza kuwa ameanza kufanya mazoezi mepesi ambayo yatamfanya aweze kurejea kwenye kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England chini ya Jurgen Klopp.

 

Taarifa kutoka Liverpool imeeleza kuwa beki huyo anaendelea vizuri na upasuaji wake ulikwenda vizuri jambo ambalo limemfurahisha Klopp ambaye amesema kuwa wanatarajia kuwa na habari njema hivi karibuni.

 

Liverpool inapambana kutetea taji la ligi ikiwa inawakosa nyota wake wengi ambao ni mabeki ikiwa ni pamoja na Joe Gomez, Fabinho ambao wanasumbuliwa na majeraha.

 

 

The post Van Dijk Atajwa Kuanza Mazoezi Mepesi Liverpool appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand