-->

Type something and hit enter

On
 JUMA NATURE amewashauri wasanii wa Bongofleva wanaotamba kwa sasa, Nandy na Zuchu, akiwataka kutobweteka na mafanikio waliyopata. Amewataka watenge muda wa kukutana na watangulizi wao akiwemo msanii Lady Jay Dee.

 

Nature ambaye ni msanii wa muziki wa Bongofleva wa siku nyingi nchini Tanzania amewapa ushauri wawili hao wakati akizungumza na Mwananchi Digital lililotaka kusikia maoni yake baada ya wasanii hao kushinda tuzo za Afrimma.


Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

 

Katika tuzo hizo Zuchu amEshinda kipengele cha msanii bora anayechipukia huku Nandy akishinda kipengele cha msanii bora wa kike Afrika Mashariki. Msanii Diamond Platnumz alishinda kipengele cha msanii bora wa kiume Afrika Mashariki.

 

Akizungumzia ushindi wao, Nature amesema wana kipaji, “asikuambie mtu ukikubalika katika tuzo za kimataifa kama Afrimma wewe una kipaji na sio cha kukipuuza na kukubali kulewa sifa, ninachowasihi wadogo zangu Zuchu na Nandy wasichukulie poa hapo walipofikia wakaze buti.”

 

Aliwataka watambue kuwa mtaani wanapendwa na kukubalika kuliko wanavyofikiria na kusisitiza kuwa wanapaswa kutowasahau wala kuwadharau waliowatangulia.

 

“Watenge muda wa kuwatafuta na kuchota mawili matatu kutoka kwa wakongwe wa muziki huo akiwemo Lady Jay Dee ambaye ni dada yao,” amesisitiza Nature.

 

Wakati Nature akitoa ushauri huo, Zuchu amewahi kumualika Jay Dee katika uzinduzi wa EP yake uliofanyika Aprili, 2020 kwenye ukumbi wa Mlimani City.

Click to comment
 
Blog Meets Brand