-->

Type something and hit enter

On
 BAADA ya mchezo wa kwanza wa wa ufunguzi kwenye mashindano ya Cosafa yanayofanyika nchini Afrika Kusini leo timu ya Taifa ya Wanawake ya U 17 imepoteza kwa kufungwa mabao 2-1.


Mchezo wa kwanza kwa U 17 iliyo chini ya Kocha Mkuu, Edna Lema ambaye ameweka wazi kuwa wachezaji wapo vizuri katika kupambana ili kupata matokeo chanya ilishinda kwa mabao 5-1.


Ilikuwa ni Novemba 4 dhidi ya Comoros ambapo walifanikiwa kuanza kwa mguu mzuri na kusepa na ushindi kwenye mchezo huo.


Mechi zote mbili zimechezwa Uwanja wa Oval nchini Afrika Kusini na jumla U 17 imefunga mabao sita huku ikifungwa mabao mawili.


Mashindano hayo ambayo yameanza Novemba 4 yanatarajiwa kukamilika Novemba 14.

Click to comment
 
Blog Meets Brand