-->

Type something and hit enter

On
UKIZUNGUMZIA wanamuziki wa kike wenye nguvu ndani ya Bongo Fleva kwa sasa, jina la Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’, haliwezi kukosekana.

Hii ni kutokana na kipaji kikubwa alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu cha kuimba kwa umahiri kiasi ambacho mashabiki walimaliza bando zao za kutosha kumpigia kura hili anyakue Tuzo ya AFRIMMA zilizofanyika nchini Marekani hivi karibuni.

Taarifa ya kuwa mmoja wa wanamuziki watatu kutoka nchini Tanzania na Afrika Mashariki kupata tuzo hizo zilimshtua mno Nandy, kiasi ambacho mshtuko alioupata ulitaka kuitoa roho yake kwani ni kitu ambacho hakufikiria kama atashinda.

Nandy ametwaa Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika Mashariki huku Diamond akinyakuwa Mwanamuziki Bora wa Kiume Afrika Mashariki, wakati Zuchu yeye ametwaa Tuzo ya Mwanamuziki Chipukizi Afrika.Click to comment
 
Blog Meets Brand