-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BONDIA Arnel Tinampay kutoka Ufilipino na Idd Pialali wa Tanzania wakitambiana mbele ya kamera za Global TV Online na +255 Global Radio walipofika katika ofisi za Global Group, Sinza Mori jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya utambulisho wa pambano lao la Kimataifa watakalocheza Jumamosi, Novemba 28, 2020.

 

Tinampay anasema atamtwanga Pialali mapema kwa sababu ameshamsoma anacheza kama Hassan Mwakinyo, hivyo kwake yeye kazi itakuwa nyepesi tu kumtwanga Mtanzania huyo mapema.

 

Lakini kwa upande wake Pialali anasema yeye na Mwakinyo ni mabondia tofauti na hawezi kufananishwa na bondia yeyote hapa nchini kwani ana uzoefu mkubwa na mashindano mengi na makubwa ya Kimataifa, uwezo wake Pamoja na mbinu za mwalimu wake, hivyo Mfillipino huyo asijidanganye, atamtwanga kwa KO na hatorudi tena Tanzania.

 

Shughuli itakuwa pevu pale Next door Masaki….. Tayari tikezi za pambano tayari zinauzwa kwa kiingilio cha sh 20,000 mzunguko, Sh 50,000 kawaida na Sh 100,000 kwa VIP. Tiketi hizo zinapatikana kupitia Nilipe App,Selcom ,Vunja Bei Store na Vunja Bei Toto Sinza, Shishi Food Kinondoni ,Cake City Njiapanda ya SalaSala, Kaites Louge Tabata na Dick Sound Magomeni.

 

Pambano hilo limedhaminiwa na Gazeti jipya na bora la michezo nchini…. #SpotiXtraJumanne
Pamoja na: @255globalradio

 

The post Tinampay Amtisha Pialali, Naye Aapa Kumbomoa kwa KO – Video appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand