-->

Type something and hit enter

On
 HITIMANA Thiery Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa kwa sasa timu yake ipo mapumziko kwa kuwa ligi imesimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu za taifa kwa ajili ya mechi za Afcon.


Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa wakati huu hakuna program ambayo inaendelea kutokana na ligi kusimama.


"Kwa sasa hakuna kinachoendelea kuhusu maandalizi kwa kuwa ligi imesimama hivyo ligi itakaporejea ninaamini kwamba tiutaendelea pale ambapo tuliishia," amesema.


Namungo yenye maskani yake Lindi inatumia Uwanja wa Majaliwa kwa mechi zake za nyumbani.


Ikiwa imetupia mabao saba kinara wake ni Bigirimana Blaise mwenye mabao manne.


Kwenye msimamo ipo nafasi ya 9 baada ya kucheza mechi 10 na ina pointi zake 14.

Click to comment
 
Blog Meets Brand