-->

Type something and hit enter

On
 TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, usiku wa kuamkia leo Novemba 18 imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Taifa ya Tunisia kwenye mchezo wa kuwania kufuzu tiketi ya kushiriki Afcon.


Mchezo wa leo ambao ulikuwa ni muhimu kwa Stars kushinda kwa kuwa ule wa kwanza ugenini ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 nchini Tunisia ulikuwa mgumu kwa Stars kwa kuwa walikubali kufungwa kipindi cha kwanza.

Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Zikiwa zimetofautiana dakika nane kwa kuwa mchezo wa kwanza Stars ilifungwa bao la ushindi dakika ya 18 leo Uwanja wa Mkapa imefungwa dakika ya 10.


Bao la kuongoza kwa Tunisia ambao tayari wameshafuzu michuano ya Afcon lilipachikwa kimiani na Saif Eddine Khaoul.


Iliwalazimu Stars kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao moja huku safu ya ushambuliaji iliyokuwa inaongozwa na nahodha John Bocco ikiwa haijafanya jaribio la hatari ndani ya dakika 45.


Bao la kuweka usawa na kuipa pointi moja Stars lilifungwa na Fei Toto ambaye alianzia benchi na alichukua nafasi ya Himid Mao dakika ya 47 kwa shuti kali akimaliza pasi iliyotengwa na Bocco.


Pointi hiyo moja inaifanya Stars iwe nafasi ya nne ikiwa na pointi nne baada ya kucheza mechi nne huku Tunisia ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 10.


Nafasi ya nne ipo mikononi mwa Libya yenye pointi tatu na ile ya pili ni mali ya Equatorial Guinea yenye pointi 6 kwenye kundi J.

Click to comment
 
Blog Meets Brand