-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KIUNGO mshambuliaji wa Klabu ya Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, amefanikiwa kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Azam FC Oktoba, 2020.

 

Sure Boy ametwaa tuzo hiyo akiwazidi wachezaji wenzake, beki Bruce Kangwa, kiungo mkabaji Ally Niyonzima, washambuliaji Obrey Chirwa na Prince Dube.

 

Nyota huyo amekabidhiwa tuzo hiyo na Sheikh Twalib, kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Azam FC na Dodoma Jiji uliochezwa jana Novemba 5, 2020.

 

Kwenye mchezo huo Azam FC iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 ambayo yanaifanya ipande kileleni kwa kuishusha Yanga nafasi ya kwanza baada ya kufikisha jumla ya pointi 25.

The post Sure Boy Anyakua Tuzo ya Mchezaji Bora wa Azam FC Oktoba appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand