-->

Type something and hit enter

On

Ni maajabu! Ndivyo unavyoweza kutafsiri wosia aliodaiwa kuachwa na bilionea wa Zimbabwe, Genius Kadungure ‘Ginimbi’ ambaye amezikwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika makazi yake huko Domboshava nchini humo.

Katika wosia huo imeelezwa kuwa bilionea huyo ambaye pia ni shemeji wa mzazi mwenza wa msanii maarufu nchini, Nasib Abdul ‘Diamond’, Zarina Hassan, aliagiza kuwa akifariki magari yake yote yauzwe na fedha zitakazopatikana zigawiwe kwenye vituo vinavyolea watoto maskini wanaoishi katika mazingira magumu.

Pia bilionea huyo aliyekuwa anakadiriwa kuwa na utajiri wa zaidi ya Sh bilioni 200, aliagiza nguo zake za thamani, na viatu vyote vichomwe moto. Kwa mujibu wa gazeti la The Herald la nchini humo, maagizo ya bilionea huyo, yamewaacha midomo wazi wananchi wa Zimbabwe, wafuasi wake pamoja na familia yake kwa ujumla.


Click to comment
 
Blog Meets Brand