-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BOSI wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, amesema anatarajia kuwa na mchezo mgumu mbele ya Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta kutokana na jinsi alivyoanza kwa mafanikio akiwa na timu hiyo leo Jumapili, Man United na Arsenal zitashuka katika Dimba la Old Trafford kupambana kwenye mchezo wa Premier League kuanzia saa 1:30 usiku.

 

Arsenal msimu katika Premier, imeshinda mechi tatu na kupoteza tatu, huku Man United ikipoteza mechi mbili na zote Old Trafford dhidi ya Crystal Palace na Tottenham Solskjaer alisema kuwa, Arsenal ni timu ngumu ila inafundishwa na kocha bora ambaye atawapa wakati mgumu.

 

“Kwa Arsenal siku zote kupambana nao sio kazi rahisi, sababu ni timu nzuri ambayo inaongozwa na kocha bora ambaye analijua soka vizuri.

“Kocha yeyote huwa anahitaji muda kwa kuhakikisha anakuwa na mipango yake na aina ya uchezaji wake, lakini yeye (Arteta) tayari ametwaa ubingwa na anaonekana ana kitu gani anafanya “Kila mmoja anaona anachofanya tena kwa mawazo yake na amekuwa kwenye presha kama kocha mkubwa.

 

“Ndiyo kwanza yupo mwanzo kabisa katika kazi yake ya ukocha, ila tayari ameshinda mataji na amejenga kitu kikubwa ndani ya Arsenal na ni mtu wa aina yake ambaye alikuwa anahitajika ndani ya klabu hiyo,” alisema Solskjaer.

 

The post Solskjaer Amuhofia Arteta appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand