-->

Type something and hit enter

On
 KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solksjaer, amesema makosa yaliyofanywa na mabeki wake yaliyosababisha wafungwe bao 2-1 na Instanbul Basaksehir katika ligi ya mabingwa Ulaya si ya kusameheka.

 

 

Mabeki wa United walifanya makosa ya kizembe yaliosababisha Edin Viska na Demba Ba kufunga mabao yaliyowapa ushindi Instanbul ushindi wa kwanza katika ligi ya mabingwa Ulaya.

 

Akizungumzia mchezo huo, Solksjaer amesema ni mbaya sana kuruhusu mabao ya aina ambayo ni wazi yalikuwa makosa yasiyovumilika, na ameahidi watayafanyia kazi.

 

Katika hatua nyingine Solksjaer amezipuuza fununu zinazodai kwamba kazi yake ipo mashakani kutokana na mwenendo wa timu yake huku akisisitiza kwamba ameajiriwa kutekeleza majukumu yake na anajitahidi kadiri iwezekanavyo huku akiamini uwezo wa wachezaji wake.

 

Wachezaji wa zamani wa The Red Devils akiwemo aliyekuwa nahodha Roy Keane wamekuwa wakikosoa mwenendo wa timu hiyo lakini Ole Gunnar amesema hiyo ni kazi yake na yeye anaendelea na kazi ya aliyokabidhiwa.

Click to comment
 
Blog Meets Brand