-->

Type something and hit enter

On
 SIMON Msuva nyota mzawa ambaye yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Tunisia unaotarajiwa kuchezwa Novemba 13 kwa sasa ni mali ya Wydad Casablaca.


Mzawa huyo alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Difaa El Jadida hivyo anaanza changamoto mpya ndani ya Klabu ya Casblaca kwa dili la miaka minne zote zikiwa ni za nchini Morroco.


Kwa hatua ambayo amefikia Msuva bado anastahili kupata changamoto zaidi ili aweze kuifungulia Tanzania njia za mafanikio zaidi ya hapo kwenye soka.


Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Kuondoka kwakwe kwenye timu yake ya zamani kutakuwa kumeacha alama kubwa kama wakati ule alipokuwa ndani ya Klabu ya Yanga, hayo ni maisha ya soka.


Lakini ikumbukwe kwamba hajafika hapo kwa kubahatisha hilo halipo bali ni jitihada zake binafsi pamoja na sapoti ya kila mmoja katika kumuombea dua na kuwa naye karibu.


Hata akiwa ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania, Msuva amekuwa akijitoa na kutimiza majukumu yake ili kuona kila shabiki ambaye hamuoni ndani ya ardhi ya Bongo ananufaika na mchango wake akiwa kazini.


Hili ni somo kwa wengine ambao alianza nao kazi na kufanya hivyo itawasaidia kuongeza ushindani na upana wa kikosi kwa timu ya Taifa ya Tanzania.


Nchi nyingi ambazo zinafanya vizuri kitaifa na kimataifa zimewekeza kwa wachezaji wao wengi kupata ushindani kutoka nje ya hapo walipo kwa kuwa changamoto mpya zinawajenga na kuwakomaza wachezaji ambao watakuwa wanatumika ndani ya timu zao za Taifa.


Kwa miaka ya hivi karibuni milango imeanza kufunguka ambapo na Tanzania pia ina wachezaji wengi ambao wanacheza nje ya nchi haya ni mafanikio ya mwanzo tunaamini kwamba soka letu litazidi kupasua anga.


Yote kwa yote kwa hatua ambayo umefikia, hongera Msuva endelea kupambana na kuongeza juhudi bado uwezo unao na nguvu unazo.


Wape darasa wale ambao wanapenda kufikia hatua uliyopo kwamba mafanikio sio kitu cha kufikiria muda wote bali vyote viwili vinakwenda kwa wakati mmoja kufikiria na kutenda.

Click to comment
 
Blog Meets Brand