-->

Type something and hit enter

On
 MAKOMANDOO wa Simba na Yanga Jana Jumamosi wameonyeshana ubabe pale walipoamua kuzipiga kavukavu baada ya mabishano ya kila mmoja kumtaka mwenzake aondoke getini.

 

Yanga ndiyo ilikuwa mwenyeji wa mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Benjamini Mkapa iliwakaribisha watani zao Simba ambapo kila upande ulikuwa na makomandoo wake getini.

 

Vurugu hizo zilianza baada ya makomandoo wa Simba kuwataka makomandoo wa Yanga kuondoka getini (geti kubwa la kuingilia magari) ili timu yao iingie huku tayari timu ya Yanga ikiwa imeingia ndani ambapo waligoma kwa madai kwamba wao ndio wanapaswa kukaa getini kwani ni wenyeji wa mchezo na sio wa Simba.

 

Hapo ndipo ugomvi ulipoanza, kwani makomandoo wa Simba hawakutaka mtu yeyote aliyeonekana ni wa Yanga awepo getini hapo mpaka timu yao iingie.

 

Vurugu hizo ilibidi ziamuliwe na polisi kwani makomandoo wa Simba waliwazuia hata walinzi wa usalama uwanjani ‘Steward’ kusogelea getini hapo jambo ambalo walinzi hao walilipinga huku gari la Simba likiingia kwa kuongozwa na makomandoo wao.

Click to comment
 
Blog Meets Brand