-->

Type something and hit enter

On
 IMEELEZWA kuwa Klabu ya Simba imewaondoa wapishi wao wawili ambao walikuwa wakihusika katika kuwapikia chakula wachezaji wa timu hiyo.

 

Hivi karibuni Simba imewashtua mashabiki wao kufuatia matokeo ya kufungwa mechi mbili mfululizo kwenye ligi, ilianza kwa kufungwa bao 1-0 na Prisons kule Nelson Mandela, Sumbawanga kisha iliporejea Uwanja wa Uhuru jijini Dar ikapigwa bao 1-0 na Ruvu Shooting.


 Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Awali Simba ilitangaza kuachana na kocha wa makipa Muharami Mohammed na meneja Patrick  Rweyemamu. 

 

Aidha taarifa zingine zinasema kuwa imewapiga chini Ally Shantra na Jacob ambao walikuwa kwenye kitengo cha habari.Chanzo kutoka ndani ya Simba kimeliambia Championi Jumamosi kuwa, timu hiyo imefi kia hatua ya kuwafuta kazi wapishi wawili kutokana na hofu ya hujuma kufanyika kwa wachezaji wao. 

 

Inadaiwa kuwa, Simba imeamua kuachana nao fasta na kusaka wengine ambao wanawaamini katika utendaji kazi wao kwa kuhakikisha wanawapikia chakula safi  wachezaji na benchi lao la ufundi.

 

“Simba imeachana na wapishi wao wawili kwa hofu ya hujuma kwenye ishu ya vyakula vya wachezaji, wamefanya hivi ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda safi  kwa wachezaji na timu nzima kwa ujumla,” kilisema chanzo hicho.

Click to comment
 
Blog Meets Brand