-->

Type something and hit enter

On
 UPO uwezekano mkubwa wa Kocha Mkuu mpya wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze kupitisha panga zito katika kuelekea usajili wa dirisha dogo msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Hiyo ni baada ya mchezo wa Dar es Salaam Dabi kumalizika juzi, Yanga kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.


Mabao katika mchezo huo yalifungwa na Michael Sarpong na Joash Onyango, wa Yanga na Simba, mtawalia.


Yanga ilionekana kupoteana kuanzia dakika ya 49 mara baada ya kuomba kutolewa Mghana Lamine Moro aliyepata majeraha ya goti aliyegongana na Shomari Kapombe kabla ya kutoka na kuingia Said Makapu aliyeonekana kushindwa kuziba pengo lake.


Akizungumza na Championi Jumatatu, Kaze alisema kuwa kikubwa kilichosababisha wao wapoteane katika kipindi cha pili ni kumkosa beki mzuri wa akiba wa kutokea benchi.


Kaze alisema kuwa hilo ameliona baada ya kutoka Lamine aliyeonekana ndiyo kikwazo kwa washambuliaji wa Simba. 


Aliongeza kuwa ameliona hilo huku akipanga kulifanyia kazi katika usajili wa dirisha dogo kwa kuhakikisha anakuwa na wachezaji watakaokuwa na tija katika timu.


“Nilimuingiza Makapu ambaye ndiye nilimuona yupo vizuri katika mazoezi ya siku hizi mbili tukiwa tunajiandaa na mchezo wa dabi dhidi ya Simba, lakini alipoingia alishindwa kufanya kile ambacho nilikuwa nikikitarajia.


“Pia, nilimtoa Sarpong aliyekuwa amechoka na kumuingiza Yacouba (Songne) aliyeonekana kucheza chini ya kiwango na hao ndio wachezaji waliokuwepo kwenye benchi.


“Hivyo sina wachezaji wazuri wa kutokea benchi watakaonipa matokeo mazuri, nimeliona hilo, nimepanga kulifanyia kazi na hivi karibuni mtaona,” alisema Kaze.

Click to comment
 
Blog Meets Brand