-->

Type something and hit enter

OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB

Cristiano Ronaldo amerejea kutoka kwenye karantini kufuatia kukutwa na virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 19 na kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 wa Juventus dhidi ya wenyeji, Spezia kwenye mchezo wa Serie A jana Uwanja wa Orogel -Dino Manuzzi, Cesena.
Ronaldo aliyekosa mechi nne zilizopita, alifunga dakika ya 59 akimalizia pasi ya mfungaji wa bao la kwanza Alvaro Morata na dakika ya 76 kwa penalti dakika ya 14 baada ya Federico Chiesa kuangushwa na Paolo Bartolomei.
Mabao mengine ya Juventus yalifungwa na Alvaro Morata dakika ya 14 na Adrien Rabiot dakika ya 67, wakati bao pekee la Spezia lilifungwa na Tommaso Pobega dakika ya 32
 


Click to comment
 
Blog Meets Brand