-->

Type something and hit enter

On
 Italia (AFP).Nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo amekutwa hana virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo, lakini klabu za soka za Serie A nchini Italia-- Atalanta, Sassuolo, Crotone na Parma zimetangaza maambukizi mapya.


Ronaldo alikutwa na Covid-19 kwa mara ya kwanza Oktoba 13 wakati akiichezea timu yake ya taifa ya Ureno.


Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


"Ronaldo amechukuliwa vipimo vya Covid-19. Upimaji umeonyesha kuwa hana virusi," mabingwa hao wa soka wa Italia walisema katika taarifa.


"Kwa maana hiyo, mchezaji amepona baada ya siku 19 na hatakiwi tena kujitenga nyumbani."


Mechi ijayo, Juventus itacheza na klabu iliyopanda daraja msimu huu ya Spezia kesho Jumapili, huku mechi zote zikichezwa bila ya mashabiki kuruhusiwa kuingia uwanjani.


Vinara wa Serie A, AC Milan pia walitangaza kuwa beki Matteo Gabbia, kipa Gianluigi Donnarumma na mshambuliaji Jens Petter Hauge wamekutwa na virusi hivyo ambavyo husababisha homa kali ya mapafu.

Click to comment
 
Blog Meets Brand