-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Prince Dube raia wa Zimbabwe, ameshindwa kufunga bao kwenye mechi tatu mfululizo ndani ya Ligi Kuu Bara ambazo ni sawa na dakika 270.

 

Dube alianza na moto msimu huu kwenye ligi hiyo baada ya kuifungia Azam mabao sita na kutoa asisti tano akiwa kinara wa ufungaji kwenye ligi hiyo.Baada ya kuonesha makali yake, sasa moto kama umezimika kutokana na kushindwa kufunga dhidi ya Ihefu, Mtibwa na JKT Tanzania.

 

Mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa ameonekana kupaniwa na mabeki wa timu pinzani baada ya kuutambua ubora wake, juzi Ijumaa aliwekewa ulinzi mkali na JKT Tanzania na kushindwa kufurukuta.

 

Kocha wa JKT Tanzania, Abdallah Mohamed ‘Bares’, aliliambia Spoti Xtra kuwa: “Tuliwapa majukumu maalum wachezaji wetu ya kujua ni jinsi gani watacheza na Dube, hatimaye wamefanikisha.

 

“Ukweli ni kwamba ni mchezaji mwenye bahati ya kuzitumia nafasi ambazo anazipata, lakini kwenye mchezo huu tulijaribu kumnyima hizo nafasi.”

HUSSEIN MSOLEKA NA LEEN ESSAU

The post Prince Dube Akwama Kwa Dakika 270 Bongo appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand