-->

Type something and hit enter

On
 IMEELEZWA kuwa mmoja kati ya waamuzi hawa wanne atakuwa ni mwamuzi wa kati kwenye mchezo wa dabi ya Kariakoo kati ya Yanga dhidi ya Simba utakaochezwa Novemba 7, Uwanja wa Mkapa.


Bodi ya Ligi Tanzania kupitia kwa Mtendaji wake Mkuu, Almas Kasongo uliweka wazi kuwa kwenye mchezo huo jumla ya waamuzi ambao watatumika ni sita na kati ya hao wawili watakaa katika magoli mawili.

Taarifa zinaeleza kuwa miongoni mwa majina ambayo yapo mezani kwa sasa ni pamoja na Martin Saanya,Emmanuel Mwandembwa, Elly Sassi na Abdallah Mwinyimkuuu ambapo kati ya hawa mmoja atakuwa mwamuzi wa kati.

Mambo yanatajwa kuwa magumu baada ya Shomari Lawi mwamuzi ambaye alipewa kipaumbele cha kusimamia dabi hiyo kufungiwa mwaka mzima kujihusisha na masuala ya soka baada ya kuelezwa kuwa alishindwa kuumudu mchezo wa ligi kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Simba.

Pia Jonesia Rukya kwa sasa yupo nje baada ya kufanyiwa upasuaji hivyo itakuwa ngumu kwake kukaa kati kwenye mchezo huo ambao presha yake ni kubwa.

Taarifa hiyo iliweka wazi orodha ya majina wanaotarajiwa kuwa waamuzi wa pembeni ambao ni pamoja na Frank Komba, Arnold Bugado na Mohamed Mkono.

"Mwamuzi wa awali alikuwa Shomari hivi karibuni amefungiwa na bodi ya ligi hivyo kumekuwa na ugumu kidogo wa kujua nani atakuwa mwamuzi wa kati. Wengine ambao wanatajwa ni pamoja na Saanya,Mwandembwa,Sassi na Mwinyimkuu ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa mwamuzi wa kati," ilieleza taarifa hiyo.

Click to comment
 
Blog Meets Brand