-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

Bondia wa ngumi za kulipwa Bongo, Idd Pilali hatimaye wikiendi iliyopita alikutana kwa mara ya kwanza na mpinzani wake, Arnel Tinampay kwenye (Face Off) iliyofanyika kwenye uwanja wa Urafiki zamani Kinesi, uliopo Sinza Dar, ikiwa ishara ya kuelekea Novemba 28 katika usiku wa Dar Boxing Derby kwenye ukumbi wa Next Door Arena.

 

Pialali na Tinampay walikutana kwenye uwanja huo na kushuhudiwa na maelfu ya mashabiki ambao walijitokeza uwanjani hapo kushuhudia usiku mwingine wa Dar Boxing Derby ambao uliwakutanisha mabondia mbalimbali, huku pambano kubwa na lililowavutia wengi ni lile la Francis Miyayusho Chichi Mawe aliyemchapa Deo Samweli kwa TKO ya raundi ya nane.

Akizungumza mbele ya mashaiki Pialali alitamba kumchakaza vibaya Tinampay raia wa Ufilipino: “Huyu ameyakanyaga, alikuja mzima atarejea kwao akiwa maiti. Nimefanya mazoezi mengi na makali kwa ajili yake, sitaki kupata ushindi wa makandokando, nataka ushindi  kweli.”

 

Kwa upande wa Tinampay ambaye hakuwa na maneno mengi alisema: “Pialali ni bondia mzuri, lakini mimi nimekuja tena Tanzania kuonyesha mchezo mzuri, tukutane Novemba 28.”

Tinampay alitua nchini Novemba 21 kwa ajili ya pambano lake hilo huku akitamka wazi kuwa Pialali ana uwezo mkubwa wa kutembea ndani ya ulingo lakini haiwezi kumtisha kwa kuwa yeye ni mzoefu na moja kati ya mabondia wakali duniani.

 

Mbali ya pambano hilo mapambano mengine ya utangulizi pia yatakuwepo, Adam Chiga anatarajia kucheza dhidi ya Adam Kipenga wakati Ramadhan Shauri akitarajia kucheza dhidi ya Salehe Mkalekwa.

Mkongwe Japhet Kaseba atavaana na Iman Mapambano, SelemanKidunda kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ yeye ataonyesha ubavu na mkongwe Said Mbelwa.

 

 

Wakati Ismail Galiatano kutoka pia JWTZ atazichapa na Mustafa Dotowa upande wa kinadada bondia Stumai Muki atamaliza ubishi dhidi ya mkali Lulu Kayage mapambano hayo yamedhaminiwa na Gazeti laSpoti Xtra, +255 Global Radio, DSTV, Plus TV, Uhuru Fm, Clouds Media, Precision Air, Smart Gin na Kebby Hotel.

Story na Ibrahim Mussa na Issa Liponda

The post Pialali, Tinampay Wakutana appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand