-->

Type something and hit enter

On
 NAHODHA wa Klabu ya Manchester United, Harry Maguire anaamini kuwa kinachoitesa  kwa sasa timu hiyo ni kupitia kipindi cha mpito cha kupingwa na baadhi ya watu wenye wivu wa kuona mafanikio ya haraka ndani ya timu hiyo.

Jana Novemba 7, Maguire alikuwa kwenye kikosi cha Manchester United kilichoibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Everton kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Goodison Park.

United ilishinda mchezo huo baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Instanbul Basaksehir kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya jambo ambalo linampa wakati mgumu Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskajer ambaye yupo kwenye presha kubwa kwamba  huenda akafutwa kazi.

Ushindi huo wa United ambao ulipatikana kupitia kwa Bruno Fernandes dakika ya 25 na 32 akipundua lile moja lililofungwa na Bernard wa Everton dakika ya 19 na lile la tatu lilifungwa na Edinson Cavan dakika ya 90 aliyefunga bao lake la kwanza akitokea benchi kuchukua nafasi ya Anthony Martial dakika ya 82.


Maguire amesema:-"Nipo hapa kwenye timu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu na nimeona kuna suala la kupingwa kwetu kutokana na aina ya matokeo ambayo tunayapata hilo lipo wazi.

"Unaweza kujiuliza kwa nini? Kwa sababu sisi ni timu kubwa na tuna uwezo mkubwa suala la kupingwa huwezi kuzuia,".

Click to comment
 
Blog Meets Brand