-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mkongomani, Chris Mugalu, amerejesha matumaini kwenye kikosi cha timu hiyo katika kuelekea Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga, Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Mkongomani huyo alikuwa nje ya uwanja kwa michezo mitatu akiuguza maumivu ya nyonga ambayo ni dhidi ya Tanzania Prisons, Ruvu Shooting na Mwadui FC.

Daktari mkuu wa timu hiyo, Yassin Gembe, amesema mshambuliaji huyo amepona kabisa na suala la kucheza Jumamosi dhidi ya Yanga lipo chini ya kocha mkuu, Sven Vandenbroeck.

Gembe aliongeza kuwa, muda wote ambao Mugalu alikuwa nje akiuguza maumivu, alikuwa akifanya mazoezi binafsi chini ya uangalizi wa kocha wa viungo, Adel Zrane.“

 

Mugalu alipona maumivu yake muda mrefu na alikuwa akifanya mazoezi binafsi chini ya uangalizi wa kocha Adel kabla ya kuungana na wenzake ili kumuongezea fi tinesi ya kutosha,” alisema Gembe.

 

Katika mchezo wa jana dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar, katika kuonesha kwamba amepona, Mugalu aliingia uwanjani dakika ya 62 kuchukua nafasi ya John Bocco.

STORI: WILBERT MOLANDI

The post Mugalu Arejesha Matumaini Simba SC appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand