-->

Type something and hit enter

On


SEXY lady kunako anga la Bongo Fleva, Karen Habash ‘Malkia Karen’ anasema kuwa, hakuna maisha anayoyachukia jumla kama ya uhusiano wa kimapenzi.


Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Malkia Karen anasema kuwa, aliwahi kupitia maisha magumu mno ya uhusiano wa kimapenzi hadi kufikia hatua ya kujiona kuwa hafai kwa mpenzi wake hivyo kwa sasa ameamua kuwa single (kuishi mwenyewe bila mpenzi) na kuendelea na maisha yake.


“Asikwambia mtu, mapenzi yanauma jamani, nilipitia msoto kwa mpenzi wangu hadi nilijiona hata sifai tena, lakini nilipiga moyo konde na kuamua kufanya uamuzi mgumu na mpaka sasa ninafurahia maisha ya kuwa single,” anasema Malkia Karen ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa miondoko ya Singeli unaokwenda kwa jina la Sina akiwa na Meja Kunta.Click to comment
 
Blog Meets Brand