Mondi, Zuchu Waonyeshana Mahaba Live - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mondi, Zuchu Waonyeshana Mahaba Live


 WAKATI wakiwa angali hawajakitegua kitendawili cha kuwa ni wapenzi au la, staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zuhura Othuman ‘Zuchu’ wameonesha mahaba live kupitia mitandao yao ya kijamii.

 

ISHARA KAMA ZOTEAMANI

limefuatilia kwa ukaribu nyendo za wawili hao na kubaini hivi karibuni, waliamua kutupia ishara dhahiri zinazoonesha kwamba wanapendana.

Akiwa safarini kuelekea Malawi kwenye shoo, Diamond au Mondi alitupia kali za Zuchu kwenye kipengele cha Insta Story ambapo alisindikizia picha hizo kwa emoji za mapenzi.

 

AONGEZA MAHABA…

Kama hiyo haitoshi, alikwenda kwenye ukurasa wa Instagram wa Zuchu na kumwaga emoji za makopakopa kwenye picha mbalimbali ambazo mrembo huyo alikuwa ameziposti.Lakini kwa upande wake Zuchu naye hakuwa na hiyana naye alikwenda kwenye kipengele cha Insta Story na kurudishia posti (kuriposti) ya Diamond aliyokuwa ameiposti kuonesha picha za Zuchu.

 

MASWALIKwenye moja ya mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni na magazeti Pendwa, Zuchu alisema ukaribu wake na Diamond ni wa kikazi lakini pia akasema Mondi hakuwawi kumtongoza.

 

“Ukaribu wangu na boss wangu Diamond Platnumz ni kwa ajili ya kazi, anatumia muda mwingi kuni-promote. Hajawahi hata kunionyesha dalili za kunitaka, he is like brother to me. Ni ngumu sana kucheza vile na mtu ambae unamuheshimu, akini nashukuru Boss Sallam SK alisaidia kunifanya niwe Comfortable,” alisema Zuchu.

 

NINI MAANA YAKE?

Ukiangalia hapo utangundua kuna mstari Zuchu ameonesha kwamba Mondi hajawahi kuonesha kumtaka hivyo maswali yameibuka kwamba je, akionesha atakuwa tayari?

 

MAKABRASHA YA AMANI

Kwenye makabrasha ya Amani, kuna taarifa mbalimbali ambazo zinadhihirishwa na ushahidi wa picha kwamba mara kadhaa Zuchu amekuwa akionekana nyumbani kwa Mondi, Mbezi Beach jijini Dar.

 

Kama hiyo haitoshi, zipo picha ambazo ziliwahi kuvuja na kudaiwa kuwa mrembo huyo alikuwa chumbani kwa Mondi.Mbali na hizo, zipo picha mbalimbali ambazo zinamuonesha Mondi akiwa kwenye mizunguko na mrembo huyo wakiwa kwenye mavazi ya kufanana.

 

TUJIKUMBUSHE

Zuchu alianza kuzua gumzo kufuatia Mondi kuonesha ukaribu mkubwa kwa msanii huyo tangu amsaini kwenye lebo yake ya Wasafi Classic Baby (WCB).

 

Zuchu alipata ukaribisho wa maana na kuandaliwa shoo kubwa kubwa huku pia naye akionesha ubora wake kwenye nyimbo zake kwani ziliweza kufanya vizuri kwa kupata watazamaji wengi.Tangu aingie Wasafi, Zuchu ameonekana kuwafunika wasanii wengi waliokuwa wametangulia kusainiwa na lebo hiyo.

 

TUTEGEMEE LOLOTE

Tangu Mondi aachane na Tanasha aliyezaa naye mtoto mmoja, hajawahi kutangaza mpenzi mpya hivyo kama mambo yatakuwa sawa na wawili hao wakaelewana basi lolote linaweza kutokea.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz