-->

Type something and hit enter

On
 MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji amesema kuwa hela zote za usajili yeye anatoa kwa kuwa timu hiyo haina hela.

Jana, Novemba 15 Dewji alizungumza na Waandishi wa Habari na kuweka bayana mpango wa timu hiyo ni kufika mbali kimataifa.

Dewji ameweka wazi kuwa miongoni mwa wachezaji ambao ametoa pesa zake na kuwasajili ni pamoja na kiungo mshambuliaji Luis Miquissone pamoja Clatous Chama.


Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Suala la Chama lilivuta hisia za wengi ambapo habari zilikuwa zinaeleza kuwa yupo kwenye rada za Yanga jambo ambalo ameliweka wazi kwa kusema kuwa nyota huyo ana mkataba na Simba mpaka 2022.

Dewji amesema:-"Bado hatujaandaa bajeti ya usajili, hivi sasa tunasubiria mapendekezo ya wachezaji ambao kocha anawahitaji, lakini Simba haina hela ila mimi ndio natoa hela.


"Katika hilo la usajili nimepanga kuja na utaratibu mpya wa usajili wa wachezaji wetu kwa kuwapa mikataba mirefu kwa kuanzia miaka minne kwenda mbele," amesema.

Click to comment
 
Blog Meets Brand