-->

Type something and hit enter

On
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji amesema suala la Simba kuwa inamuwania kiungo nyota wa Yanga, Mukoko Tonombe ni propaganda zilizotengenezwa.


Dewji amesema Simba haijawahi kumjadili Mukoko na wala haina habari naye kama inavyoelezwa mitandaoni.


Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dewji amesema kila suala la usajili wa Simba, ni mapendekezo ya kocha.


"Kocha ndiye anependekeza mchezaji gani anatakiwa, huyo mchezaji hatujawahi kumjadili," alisema.


Hata hivyo, Dewji alikiri kuwa Kocha Sven van der Broeek amependekeza kusajiliwa kwa kiungi mkabaji kutokana na Gerson Fraga kuwa majeruhi kwa muda mrefu sasa.


Kutokana na hilo, Dewji aliendelea kusisitiza kwamba suala lao la kumsajili kiungi mkabaji litakuwa ni siri.


"Hiyo ni siri, si kwamba tunazihofia timu za hapa ndani. Lakini tunahofia pia hata zile za nje ya Tanzania kwa kuwa kutokana na mwendo mzuri wa Simba, kumekuwa na ushindani mkubwa sana."


Hivyo karibuni kulizuka taarifa kwamba kutokana na Yanga kuonekana kutaka kumsajili Cleotus Chama kutoka Simba, Msimbazi nao wameamua kuhamishia mashambulizi kwa Mukoko raia wa DRC maarufu kama Ticha.

Click to comment
 
Blog Meets Brand