-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

Mabingwa wa Tanzania  timu ya Simba leo Novemba 29, imefanikiwa kushinda mchezo wake wa kwanza kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ugenini, kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Plateua United, mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja New Jos, Nigeria wenye uwezo kuchukua watazamaji 40,000.

12

Goli pekee la wekundu wa msimbazi liliwekwa kimiani na mchezaji wa kimataifa wa Zambia, Cloutus Chama dakika ya 53  kipindi cha pili, akipokea  pasi ya Luis Miquissone ambaye alikuwa ni hatari kwa mabeki wa Plateau United.

 

Mchezo huo uliochezwa  uligubikwa na matukio mengi kutoka  kwa wenyeji wakiwa na lengo na kuwatoa Simba mchezoni,  mojawapo ya tukio kubwa ilikuwa kugoma kutoa kibali mechi hiyo kuonyeshwa kwenye runinga kupitia kituo chochote cha habari.

 

Baada ya ushindi huo ambao  kikosi cha Simba kinarejea nchini  kujiandaa na mechi ya marudiano itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es salaam, Desemba 6.

The post Mnyama Anguruma Nigeria, Ampiga Plateua Utd 1-0 appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand