-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

NYOTA  wa timu wa kimataifa wa Argentina,  Lionel Messi, amevunja ukimya na kueleza bayana kuwa amechoshwa na zigo la lawama analotupiwa ndani ya  klabu ya Barcelona yenye maskani yake Catalunya nchini Hispania.

 

Messi amesema kuwa amekuwa akipewa lawama kwa kila matatizo yanayotokea Barcelona, kauli hiyo imekuja baada ya aliyekuwa wakala wa Antoine Griezmann, Eric Olhats, kudai Mfaransa huyo amekuwa katika wakati mgumu ndani ya klabu kwa sababu ya Lionel Messi.

 

Olhats amemtuhumu Messi kwa kuwa mtu mwenye ushawishi  mkubwa ndani ya Barcelona, na kumfanya Griezmann kuwa kwenye wakati mgumu wa kuzoea mfumo wa timu hiyo, tangu alivyotua ndani ya timu hiyo mwaka uliopita.

 

Ukiwa umebaki  mwaka mmoja katika mkataba wake ndani ya Barcelona, Messi aliwahi kujaribu kufuatilia kifungu kinachombana yeye kushindwa kuondoka Barcelona kama mchezaji huru na kuamua kubaki  ili kuepusha malumbano na klabu hiyo.

 

Barcelona inapitia kipindi kigumu cha machafuko tangu Bayern Munich ilipoidhalilisha timu hiyo kwa kuipa kipigo cha aibu cha goli 8-2 katika michuano ya  Uefa Champions League hatua ya robo fainali msimu uliyopita.

 

Kauli hii ya Messi inachochea uvumi wa kuondoka hasa baada ya kocha wa Manchester City Pep Guardiola kuongeza mkataba na kuwepo uwezekano mkubwa wa kutimka kwa kocha wake huyo wa zamani.

 

The post Messi Achoshwa na Lawama Barcelona appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand