-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, amewachambua washambuliaji wake wote, huku akidai kuwa bado hana chaguo la kwanza na kudai kwamba atawatumia kulingana na michezo husika.

 

Simba kwa sasa ina washambuliaji wa kati wanne ambao ni Meddie Kagere, John Bocco, Chris Mugalu na Charles Ilanfya ambao kwa pamoja wameifungia timu hiyo mabao 10 katika michezo ya Ligi Kuu Bara kabla ya mchezo wa juzi dhidi ya Kagera Sugar.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Sven alisema mpaka sasa hana mshambuliaji tegemeo au chaguo la kwanza katika kikosi chake ila hupenda kuwatumia washambuliaji hao kulingana na aina ya wapinzani ambao hukutana nao.

 

“Siwezi kusema kuwa chaguo langu namba moja ni nani, ila kinachotakiwa kufahamika kuwa wote ni washambuliaji wangu na nitawatumia kulingana na aina ya mechi ambayo ipo mbele yetu.

 

“Wote ni washambuliaji wazuri, ukiwaangalia wanavyocheza utagundua kuwa ni wachezaji wa aina gani, tunafurahia kuwa na washambuliaji wa aina yao na naamini wataisaidia timu kupata mafanikio zaidi,” alisema kocha huyo.

MARCO MZUMBE, DAR ES SALAAM

The post Mbelgiji Simba Awachambua Mastaa Wake appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand