-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA mkuu wa timu ya Kagera Sugar, Mecky Maxime, ametamba kuibuka na ushindi kwenye mchezo dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa leo Jumatano jioni kwenye Dimba la Uhuru jijini Dar.

 

Kagera Sugar hawana mwenendo mzuri kwenye Ligi Kuu Bara (VPL), wakifanikiwa kushinda mechi mbili, sare mbili na wamepoteza mechi tano, leo watakuwa na kibarua kigumu mbele ya mabingwa watetezi Simba SC ambao wanapambana kurejea kileleni mwa ligi hiyo.

Akizungumza na Championi Jumatano, Maxime amesema: “Ninaamini nina kikosi bora, kupata matokeo yasiyoridhisha ni upepo ambao unazikuta timu zote, vijana wangu wapo tayari kuwakabili Simba, tunawaheshimu ni timu bora lakini hilo halituzuii kupambana kwa ajili ya pointi tatu.”

Kagera Sugar inashika nafasi ya 16, kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi nane baada ya kushuka dimbani kwenye mechi tisa huku Simba wakiwa nafasi ya tatu wakikusanya pointi 16 kwenye mechi nane walizoshuka dimbani.

Stori: Hussein Msoleka, Dar es Salaam

The post Maxime Aitangazia Kiama Simba appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand