-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MANCHESTER United ipo kwenye mchakato wa kuachana na wachezaji wanne katika dirisha dogo la Januari, mwakani ili kubalansi kwenye masuala ya mapato.

 

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa wachezaji ambao wako mbioni kuagwa ni Phil Jones, Timothy Fosu- Mensah, Sergio Romero na Marcos Rojo.

 

Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer amekuwa hawapi nafasi wachezaji hao na inavyoonyesha tayari hawamo kwenye mipango yake.

United pia itaachana na mshambuliaji Odion Ighalo ambaye alikuwa akicheza kwa mkopo akitokea Shanghai Shenhua, mkataba wake ukiwa unamalizika Januari, mwakani.

 

Kuondolewa kwa wachezaji hao ni kupunguza matumizi ya fedha ili kama kutakuwa na uwezekano wafanikishe mchakato wa kumsajili winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho

ambaye wamekuwa wakimuwania kwa muda.

 

Fosu-Mensah mkataba wake unaelekea ukingoni kama ilivyo kwa Romero na Rojo.

Wachezaji wote hao majina yao hayamo katika orodha ya timu hiyo wanaotakiwa kucheza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

MANCHESTER, England

The post Man Utd kutema Wanne Dirisha Dogo appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand