-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA wa Arsenal, Mikael Arteta,  amevunja mwiko baada kushinda  dhidi ya Manchester United kwenye mechi ya ligi  ya Uingereza kwenye uwanja wa Old Trafford, tangu walipofanya hivyo mwaka 2006 ikiwa imepita miaka 14.

 

Arsenal usiku wa jana walifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 kwa mkwaju wa penati iliopigwa na nahodha Pierre-Emerick Aubameyang baada ya Pogba kucheza faulo  kwenye eneo la hatari.

 

Benchi la ufundi la United bado limeshindwa kuwachezesha kwa pamoja Bruno Fernandes na Paul Pogba na timu ilionekana kukosa uwiano eneo la kiungo hivyo kuwapa nafasi viungo wa Arsenal kutawala muda mwingi wa mchezo na kutengeneza nafasi nzuri za kufunga.

 

Hata mabadiliko aliyokuwa anayafanya kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer yalionekana kushindwa na kuzidi kuharibu aina yao ya uchezaji na kuonyesha dhahiri kuzidiwa mbinu na kocha Arteta.  Arsenal imepaa hadi nafasi ya tisa na alama 12.

 

Huu ni mwanzo mbaya wa ligi kwa United kwenye uwanja wao nyumbani baada ya kupoteza mechi tatu na sare moja, na kuzidisha shinikizo la kufukuzwa kwa Solskajer ambaye timu hiyo inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi.

The post Man United Yachezea Kichapo Dhidi ya Arsenal appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand