-->

Type something and hit enter

On
 ANAANDIKA Saleh Jembe

 KATIKA hili suala la Senzo (Mbatha) na Mbaga (Hashim) kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za upangaji matokeo (match fixing) ni vizuri sana TUKAHESHIMU jeshi lenyewe na wahusika wenyewe.


Kwanza:
Senzo na Mbaga ni watuhumiwa, bado hawajahukumiwa na tuendelee kuwa na subira badala ya kuingiza ushabiki wa Uyanga na Usimba.

Naona wengine wanawatetea na wengine wanawakandamiza. Vizuri tulipe nafasi jeshi hilo kupitia wataalamu wake ili tupate majibu sahihi.

Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Pili:

Tuache propaganda katika hili, kwamba Senzo anataka kufukuzwa, na kadhalika. Anayesema anahusishaje na tuhuma za upangaji matokeo. Msizushe maneno kwa jeshi lenyewe au watuhumiwa.

Tatu:
Tupunguze kusema maneno yasiyo na ukweli ili mradi tunaweza kuandika. Jeshi la Polisi litatoa majibu na mwisho tutapata uhakika na si kila mmoja kusema analojua.

Match fixing ni adui wa mpira wetu na duniani kote. Kama polisi wanafanya uchunguzi tuwape muda ili mwisho uwe sahihi na usio na shinikizo kwa maana ya kuwa tunataka majibu ya haki nini haki ili tujue ukweli WALIHUSIKA kweli au zilikuwa HISIA tu.

Click to comment
 
Blog Meets Brand