-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MSHAMBULIAJI wa KMC, Relliants Lusajo, ameweka wazi kuwa mikakati yake msimu huu ni kuifungia timu hiyo mabao yasiyopungua 15 katika Ligi Kuu Bara, huku akiamini yataisaidia timu hiyo kufanya vizuri.

 

Lusajo amejiunga na KMC msimu huu akitokea Namungo ambapo msimu uliopita alimaliza ligi akifunga mabao 13, huku msimu huu akiwa na KMC amefunga mabao matatu katika michezo mitano aliyoichezea timu hiyo.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Lusajo alisema: “Malengo yangu ni kufunga mabao mengi iwezekanavyo, sitaki kuweka malengo niwe mfungaji bora ila nahitaji nifunge mabao mengi yasiyopungua 15 ambayo naamini yataisaidia timu yangu katika kujiweka kwenye nafasi nzuri.

 

“Msimu huu utakuwa na ushindani wa mabao kwa watu wengi kwa kuwa kuna ongezeko la washambuliaji wengi bora ambao licha ya kuwa bado hawajafunga, lakini naamini huko mbele watafunga sana na kuleta ushindani.

 

”Lusajo mbali na kuwa tegemeo kwenye Ligi Kuu Bara, pia anatazamiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Namungo kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

The post Lusajo Aahidi Mabao 15 Ligi Kuu appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand