-->

Type something and hit enter

On
 BEKI wa kati wa klabu ya Liverpool, Joe Gomez, ameripotiwa kupata majeraha makubwa na anatazamiwa kukaa nje kwa muda mrefu.

 

Gomez ameumia akiwa katika  timu ya taifa ya England, inayojiwinda na michezo kadhaa wiki hii, ukiwemo ule wa kirafiki dhidi ya North Ireland utakaopigwa jana (Alhamisi) Novemba 12, 2020, ambapo kocha mkuu wa  England, Gareth Southgate, amesema ”majeraha yake ni makubwa lakini bado sifahamu itamchukua muda gani kukaa nje ya uwanja.  Jambo hili limenihuzunisha sana, kwa kuwa alikuwa sehemu ya mipango yangu.”


Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

 

Kwa  Liverpool na kocha wao, Jurgen Klopp, taarifa hiyo si nzuri hata kidogo, kwa kuwa safu yake ya ulinzi imekumbwa na majeruhi wengi yanaowalazimu baadhi ya nyota wake kutoonekana kwa muda mrefu uwanjani, akiwemo Virgil van Dijk na kiungo Mbrazil ambaye amekuwa akichezeshwa katika safu ya ulinzi kama mbadala wa Van Dijk.

 

Kukosekana kwa wachezaji hao watatu muhimu katika kikosi cha Liverpool —  Van Dijk, Fabinho na Joe Gomez — kunauweka ubingwa rehani ubingwa walioutwaa msimu wa 2019-2020.

Click to comment
 
Blog Meets Brand