-->

Type something and hit enter

OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB

MSHAMBULIAJI Robert Lewandowski akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia Bayern Munich 
mabao mawili dakika ya 21 kwa penalti na 88 akimalizia pasi ya Javi Martínez katika ushindi wa 6-2 dhidi ya wenyeji, FC Salzburg kwenye mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Red Bull Arena. Mabao mengine ya Bayern Munich yalifungwa na Rasmus Kristensen aliyejifunga dakika ya 44, Jerome Boateng dakika ya 79, Leroy Sane dakika ya 83 na Lucas Hernandez dakika ya 90 na ushei, wakati ya FC Salzburg yalifungwa na Mergim Berisha dakika ya nne na Masaya Okugawa dakika ya 66. Kwa ushindi huo, bayern Munich inafikisha pointi tisa na kuendelea kuongoza kundi kwa ponti tano zaidi ya Atletico Madrid inayofuatia 


Click to comment
 
Blog Meets Brand