-->

Type something and hit enter

On

ZIKIWA ni wiki kadhaa zimepita tangu Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, William Lyimo ‘Billnass’ na mchumba wake Faustina Charles ‘Nandy’ waachie colabo ya wimbo wao wa Do me, ngoma hiyo imeonekana tishio baada ya kushika namba moja kwenye platifomu zote za muziki Afrika mashariki.

 

Akizungumza na AMANI Billnass alisema wanamshukuru Mungu pamoja na mashabiki wao kwa sapoti wanayozidi kuwapa bila kuchoka.


 

Alisema kitendo cha singo hiyo kutrend mfululizo kwa zaidi ya wiki mbili sio jambo dogo.“ Kwanza kabisa tumekuwa namba moja trending kwa wiki mbili mfululizo, lakini pia hivi karibuni tumeingia kwenye chati kubwa ya muziki kwenye patform zote Afrika mashariki.

 

“Hii yote ni kwa sababu ya upendo wa mashabiki zetu kwetu, naomba waendelee hivyohivyo wasituchoke, kwa sababu tumepanga kuendelea kuwaletea burudani nzuri zaidi,” alisema BillnassClick to comment
 
Blog Meets Brand