-->

Type something and hit enter

On
 EDNA Lema, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 17 amesema kuwa shukrani kubwa ni kwa Mungu pamoja na wachezaji kujituma bila kusahau sapoti ya mashabiki pamoja na Serikali.


Kwenye mchezo wa fainali ya mashindano ya Cosafa iliyofanyika jana Novemba 14 nchini Afrika Kusini Tanzania iliibuka na ushindi wa jumlajumla baada ya kushinda kwa penalti 4-3 dhidi ya Zambia.


Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulichezwa  Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini,dakika 90 za mwanzo zilikamilika kwa Tanzania kuwa nyuma kwa bao 1-0.

Katika dakika tano za kufidia muda uliopotea katika matukio mbalimbali dakika ya 90+4′ Tanzania ilipata penati baada ya mchezaji wake kufanyiwa madhambi ndani ya boksi. Tanzania ilifanikiwa kusawazisha kupitia penati hiyo iliyopigwa na Koku Kipanga mpaka mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho, Tanzania 1-1 Zambia.


Edna amesema:"Aina gani ya matokeo, aina gani ya ushindi shukrani kwa Mungu ambaye amekuwa pamoja nasi na kutupigania, haikuwa kazi nyepesi ila tumefanikiwa.


"Mashabiki wamekuwa nasi bega kwa bega, Serikali kila mmoja ni ushindi wake huu na Taifa kiujumla,".

Click to comment
 
Blog Meets Brand