-->

Type something and hit enter

On
 OLE Gunnar Solskajer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa leo Novemba Mosi ana mtihani mzito wa kusaka pointi tatu mbele ya Arsenal.


Manchester United ambayo imepoteza mechi mbili Uwanja wa Old Trafford mbele ya Crystal Palace na na Tottenham itawakaribisha tena Arsenal saa 1:30 usiku kusaka pointi tatu muhimu.

Arsenal chini ya Kocha Mkuu Mikel Arteta, imeshinda mechi tatu na kupoteza mechi tatu hivyo balaa litakuwa usiku wa leo kwa wababe hawa wawili.


Solskajer amesema:"Kwa Arsenal siku zote kupambana nao sio kazi nyepesi ni wagumu na wanahitaji akili zaidi kwa sababu ni timu nzuri ambayo inaongozwa na kocha mzuri."


Arteta amesema kuwa anaamini utakuwa ni mchezo mgumu lakini ni lazima vijana wake wacheze kwa nidhamu kupata matokeo chanya.

Click to comment
 
Blog Meets Brand