-->

Type something and hit enter

On
 KOCHA Mkuu wa Yanga,  Mrundi, Cedric Kaze, amewaongezea majukumu washambuliaji wake Michael Sarpong na Yacouba Songne ya kuwa makini katika kufunga mabao ambayo yatawapa pointi tatu hasa kwenye mechi zao za nje ya Dar.

 

Kaze ameongeza kwamba, mastraika hao wanatakiwa kuwa makini na nafasi hizo kwa sababu viwanja vingi vya mikoani haviwapi nafasi ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.


Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

 

Kocha huyo ameliambia Spoti Xtra, kuwa zoezi hilo wataanza nalo katika mechi zijazo za mikoani ili kuwa na uhakika wa kupata pointi tatu na si kubahatisha.

 

“Unajua mkoani kule viwanja havina ubora mzuri kwa hiyo inafinya nafasi ya kutengeneza mashambulizi mengi kwa mpinzani wako.

“Hivyo ni muhimu sana katika zile nafasi chache ambazo timu itatengeneza ni lazima tutumie kwa usahihi kwa ajili ya kuwa na uhakika wa kupata pointi tatu.

 

“Tukishindwa kufanya hivyo inatuweka kwenye mazingira magumu sana ya kupata kile ambacho tunakitaka, hivyo ni muhimu kwa wachezaji wangu kulizingatia hilo,” alimaliza Kaze.

Click to comment
 
Blog Meets Brand