-->

Type something and hit enter

On
 BAADA ya kumaliza kibarua chake cha kusaka pointi 12 kwenye mechi zake nne za mwanzo, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze ameingia kwenye mtengo mwingine wa kusaka pointi tisa kwenye mechi zake tatu za mwezi Novemba.

Ndani ya pointi hizo 12 alifanikiwa kupata pointi 8 na kupoteza pointi 4 baada ya kupata sare ya bila kufungana dhidi ya Gwambina FC na ile ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Simba.


Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB


Alishinda mechi mbili ilikuwa bao 1-0 Polisi Tanzania, 2-1 KMC na kumfanya akusanye jumla ya mabao manne na kufungwa mabao mawili ndani ya dakika 360 kwa sasa ana kazi nyingine tatu ambazo ni dakika 270 kwa ajili ya kufunga mwezi Novemba.

Mechi hizo itakuwa dhidi ya Namungo iliyo nafasi ya 9 na pointi 14 inanolewa na  Kocha Mkuu, Hitimana Thiery, Novemba 22, Uwanja wa Uhuru mchezo huu unaweza kufanyiwa mabadiliko kwa kuwa Namungo inamchezo wa kimataifa.


Kibarua kingine itakuwa dhidi ya vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC yenye pointi 25 baada ya kucheza mechi 10 ikiwa chini ya Aristica Cioaba itakuwa ni Novemba 25.

Kaze atafunga shughuli kwa kukutana na JKT Tanzania iliyoanza kuchangamka  kwa kuwa inashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi msimu wa  2020/21 ilikuwa dhidi ya Mwadui FC ambapo ilishinda mabao 6-1 chini ya Kocha Mkuu, Abdalah Mohamed,’Bares’  Novemba 28.

Click to comment
 
Blog Meets Brand