Kapombe: Tuisila Tafuta pa Kupitia-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

 Kapombe: Tuisila Tafuta pa Kupitia-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

 

BEKI mkongwe wa Simba, Shomari Kapombe, kamwe hatakubali kufanywa njia ya kupitia washambuliaji wa timu pinzani wa Yanga huku akiwataka watafute njia nyingine ya kupitia lakini siyo kwake.

 

Hiyo ni katika kuelekea pambano hilo la Dar es Salaam Dabi linalosubiriwa kwa hamu kubwa ambalo litapigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Mkongwe huyo aliyecheza Dar es Salaam Dabi nyingi, anatarajiwa kukutana na kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Mkongomani Tuisila Kisinda anayecheza winga wa kushoto namba 11.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kapombe alisema kuwa mechi za dabi ndizo anazozitaka yeye, hivyo hana hofu ya pambano hilo na amejiandaa vema kupambana na mshambuliaji yeyote atakayekutana naye.

 

Kapombe alisema kuwa anafahamu umuhimu mkubwa wa pambano hilo ambalo ni lazima washinde ili wapunguze idadi ya pointi walizonazo wapinzani wao Yanga waliopo kileleni wakiwa na pointi 23, Azam FC 22 na Simba wenyewe 19.

 

Aliongeza kuwa hakuna kitakachoshindikana kwao kupata ushindi katika dabi hiyo kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya chini ya Kocha Mkuu, Mbelgiji Sven Vandenbroeck.

 

“Mechi za dabi ndiyo zangu ninazozitaka kucheza, kwani tangu nikiwa na Simba nimewahi kucheza dabi zote, hivyo nina uzoefu nazo, zaidi naisubiria hiyo siku ifike haraka.

 

“Binafsi nimejiandaa vema kukabiliana na mshambuliaji yeyote nitakayecheza naye nafasi moja, mimi kama beki nitatimiza majukumu yangu ya kulinda, kuokoa na kupunguza hatari zote golini kwetu.

 

“Hivyo sitakubali nipitike kirahisi na mshambuliaji yeyote kwani katika maisha yangu ya soka sijawahi kumuogopa mchezaji yeyote zaidi ninawaheshimu,” alisema Kapombe.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post  Kapombe: Tuisila Tafuta pa Kupitia appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.