-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

 

 

KUMBE ishu ya mchezaji wa zamani wa Klabu ya Azam, Shabani Idd Chilunda kubadilishiwa timu nchini Morocco ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya ghafla ya benchi la ufundi la Klabu ya Mouloudia d’Oujda ya Morocco.

Chilunda aliripotiwa kumalizana na Mouloudia ya Morocco kabla ya baadaye kujiunga na Moghreb Atletico Tetuan na kuzua maswali mengi kwa wadau wa soka kutokana na mkanganyiko wa taarifa hizo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Thabith Zakaria ‘Zaka Zakazi’, alisema Chilunda alilazimika kusaka timu nyingine baada ya kocha mpya wa Mouloudia kumkataa.

“Chilunda alitoka Tanzania kwenda kujiunga na Mouloudia d’Oujda ya Morocco, kwa kipindi hicho kocha aliyekuwa akimhitaji alikuwa Abdelhak Benchikha lakini kabla hajaenda klabu ikabadili kocha, kocha mpya aliyekuja ni Abdeslam Ouaddou ambaye hakumtaka Chilunda.

“Hivyo ikabidi wakala wake atafute timu nyingine, ambapo baada ya mazungumzo wakafikia hiyo timu nyingine ya Moghreb Atletico Tetuan ambayo imefanikiwa kumsajili,” alisema Thabith.

Joel Thomas,

Dar es Salaam

The post  Ishu ya Chilunda Kubadilishiwa Timu Morocco Iko Hivi appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand