-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BONDIA Francis Miyeyusho jana alimtwanga kwa TKO, mpinzani wake, Deo Samweli katika pambano la raundi 8, lililopigwa Uwanja wa Kinesi uliopo Ubungo Shekilango Jijini Dar.

 

Katika pambano hilo mabondia hao walioneshana upinzani mkali mpaka raundi ya mwisho kila mmoja akimuonesha mwenzake ubabe wa kivita.

 

Raundi ya mpambano huo ikielekea ukingoni Miyeyusho aliitumia kipindi hicho kukusanya nguvu na kumshambulia mpinzani wake kwa ngumi nyingi mfululizo akiwa amembana kwenye kamba mpaka alipookolewa na mwambuzi wa mpambano huo, Pembe Ndava.

 

Kwa kipigo hicho Miyeyusho alipata ushindi wa TKO dhidi ya mpinzani wake huyo.

Jionee picha Miyeyusho akiwa na bukta ya bluu na Deo akiwa na bukta ya njano.

Sehemu ya mashabiki wakifuatilia mchezo.

Hawa nao wakiwa makini kuangalia kinachoendelea.

Wakitifuana.

Mambo yakiendelea ulingoni.

Wakiliana taiming.

Deo akijaribu kukwepa konde la Miyeyusho.

Wanaume kazini.

Mwamuzi Pembe Ndava akimuhesabia Deo baada ya kuzidiwa na masumbwi na kumfanya alegee.

Mwalimu wa mabondia Christopher Mzazi, akimshikilia bondia wake baada ya kuzidiwa huku Miyeyusho akiwa amebebwa na wasaidizi wake baada ya ushindi huo.

Miyeyusho akishangilia ushindi.         HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS WA /GPL

The post Hebu Cheki Miyeyusho Alivyomchapa Mpinzani Wake Kwa TKO Mbaya appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand